Rhumba ya COVID-19 Vaccine

Niivalie viatu gani hii rhumba? Nataka kudemka! Ndugu zangu hili suala la hii chanjo ni “double edged sword”. Ni rahisi kuliongelea katika makundi ya wataalamu wa mambo ya afya, wasomi na watu wenye kipato kizuri kama sisi, na wenye uwezo wa kufanya maamuzi binafsi. Pia sisi tuna uwezo wa kushawishi na kuwezesha baadhi ya wanafamilia wetu wapate chanjo.

Ila ningependa kujishusha daraja kidogo, nirudi kijijini kwetu kule Bugandika, mkoani Kagera. Bahati nzuri tuna umeme tayari, ila ni mpango wa serikali ya  awamu ya sita, kuhakikisha kila kijiji kina umeme kufikia mwaka 2025 (miaka 60 baadae baada ya Uhuru). Tusiongelee hata upatikanaji wa maji kwa sasa.

Ugonjwa wa COVID-19 ni kweli umesafiri kwa kasi ya ajabu mpaka kufika vijijini. Kwa hii spidi sidhani kama tuna mifumo na miundo mbinu ya kuwezesha chanjo za COVID-19 kufika mpaka vijijini kwa spidi sambamba na maambukizi.

Hata kama chanjo itakua bure kwa wananchi, napenda nivae miwani kuangalia hiyo gharama ya chanjo ya hata nusu ya Watanzania. Je, italipwa na nani na kwa muda gani? Shughuli zipi za kimaendeleo zisimamishwe ili kupata hela ya chanjo au tukope?

Nadhani kuna namna ambavyo hili suala la chanjo linaweza likawa ni kama la mjini mjini hivi, kwa watu wanaoshi mjini. Na hata huko mjini, ukifika uswazi, pita hivi. Ni kwa wale wanaoishi matawi ya juu.

Kuna umuhimu mkubwa kuangalia pia, kabla ya chanjo, ni nini kimesaidia kupunguza maambukizi ya COVID-19 mpaka sasa? Ni vitu gani vilizingatiwa na watu binafsi pamoja na ushauri wa wataalamu?

Nadhani suala la chanjo si rahisi kwa nchi zetu kulizungumzia bila kuzungumzia njia mbadala tulizotumia kudhibiti au kuzuia maambukizi. Ili hizi njia mbadala ambazo sio za bei kubwa ziende sambamba na mazungumzo ya chanjo zinazohitaji mifuko minene.

Naombeni mnisaidie kuchagua kiatu kitakachoniwezesha kudemka vizuri wakati nacheza hii rhumba ya chanjo ya COVID-19.

One thought on “Rhumba ya COVID-19 Vaccine

  1. Nadhani kabla ya kulikumbatia wazo la chanjo,tunatakiwa tuchukue muda kidogo kufanya tathmini ya yatokanayo na chanjo hii.Je wenzetu waliogundua hii chanjo hata nusu ya watu wao wamepatiwa chanjo hii ama la?Hii chanjo inaweza kuwa na dhumuni lingine hasa kwa bara la Afrika.

    Liked by 1 person

Leave a reply to Gosbert Cancel reply